Kampeni ya utunzaji wa wanyama pori

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza wanyama pori kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kampeni hii inaamini kuwa wanyama pori wakitunzwa vizuri wanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Kampeni hii inafundisha kwamba wanyama pori wanatakiwa watunzwe ili waweze kuendelea kuwepo kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae.

Kwa njia ya utunzaji wa wanyama pori, kizazi cha sasa cha watu na kizazi cha baadae kitanufaika kwa faida zitokanazo na wanyama pori.

Hivyo basi, unaalikwa kutunza wanyama pori na makazi yao ili waendelee kuwepo sasa na kwa miaka ijayo.