Kampeni ya utunzaji wa vyanzo vya maji

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kampeni hii inaamini kuwa vyanzo vya maji vikitunzwa vizuri vinaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Kampeni hii inafundisha kwamba vyanzo vya maji vinatakiwa vitunzwe ili viendelee kuwepo kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae kwa kuwa vyanzo vya maji ndio uhai wa miti na wanyama waishio duniani wakiwemo watu.

Kwa njia ya utunzaji wa vyanzo vya maji, kizazi cha sasa cha watu na kizazi cha baadae kitanufaika kwa faida zitokanazo na vyanzo vya maji.

Hivyo basi, unaalikwa kutunza vyanzo vya maji ili viendelee kuwepo sasa na kwa miaka ijayo.