Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Kampeni hii inafundisha kwamba mazingira yanatakiwa yasafishwe na kutunzwa ili yaendelee kuboresha uhai wa viumbe hai kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae kwa kuwa mazingira ndio yanayodumisha uhai wa miti na wanyama waishio duniani wakiwemo watu.

Kwa njia ya utunzaji na usafishaji wa mazingira, kizazi cha sasa cha watu na kizazi cha baadae kitanufaika kwa faida zitokanazo na mazingira bora.

Hivyo basi, unaalikwa kutunza na kusafisha mazingira ili kuboresha uhai kwa sasa na kwa baadae.