Kampeni ya utunzaji wa miti na misitu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kupanda na kutunza miti na misitu kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kampeni hii inaamini kuwa miti na misitu ikitunzwa vizuri inaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Kampeni hii inafundisha kwamba miti na misitu inatakiwa ipandwe na iliyopo itunzwe ili iendelee kuwepo kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae kwa kuwa miti na misitu ndio nguzo kuu inayoshikilia uhai wa wanyama waishio duniani wakiwemo watu.

Kwa njia ya utunzaji wa miti na misitu, kizazi cha sasa cha watu na kizazi cha baadae kitanufaika kwa faida zitokanazo na miti na misitu.

Hivyo basi, unaalikwa kupanda na kutunza miti na misitu ili iendelee kuwepo sasa na kwa miaka ijayo.