Kampeni ya kusaidia na kutetea Wazee

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea wazee kwenye mahitaji yao ya kimwili, kiroho na kijamii hasa wale wasioweza kujitegemea baada ya kuzeeka.

Kampeni hii inaamini kuwa wazee ni hazina katika jamii na bado wanaweza kuwa na mchango kwa jamii kutokana na uzoefu wa maisha. Uzee ni sawa na kurudi utotoni hivyo Wazee wanahitaji faraja na msaada hasa pale wanapokuwa hawawezi kujitegemea tena wenyewe.

Kampeni hii inahamasisha watu wote kusaidia na kuwatunza wazee ili waendelee kuishi kwa amani na furaha huku wakifurahia matunda ya kazi zao walizofanya.

Kuwasaidia na kuwatunza kunaweza kuwawezesha kuwa na amani na furaha kama watu wengine wasio wazee.

Hivyo basi, unaalikwa kusaidia na kuwatunza wazee hasa wale wasiojiweza ili kuwafanya waendelee kuona thamani ya maisha yao na kuendelea kuishi kwa amani na furaha.