Kampeni ya Kutetea Watu Wenye Ulemavu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea watu wenye ulemavu kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya walemavu wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.

Kampeni hii inaamini kuwa watu wenye ulemavu wanayo haki na nafasi sawa kama watu wengine katika jamii. Vile vile wanatamani kuishi kwa amani na furaha kwa hali ya kawaida kama watu wengine. Kwa hiyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza akawawezesha kuishi kwa furaha na matumaini kama watu wengine.

Kampeni hii inahamasisha watu wote kusaidia na kuwawezesha watu wenye ulemavu kuwa na maisha bora yanayofaa na kutamanika na binadamu yeyote wa kawaida. Msaada wako unaweza ukawa wa kiuchumi, kimawazo au maneno, kuwapa au kuwawezesha kupata mahitaji, kuwafariji na kuwatia moyo.

Kuwasaidia kujisikia na kufurahia kuwa binadamu kunaweza kuwawezesha kuwa na amani na furaha kama watu wengine.

Hivyo basi, unaalikwa kusaidia watu wenye ulemavu ili na wao waishi kwa furaha na amani kama watu wengine.