Kampeni ya Kutetea Watoto

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kuwakuza watoto kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.

Kampeni hii inaamini kuwa watoto ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae.

Kampeni hii inafundisha kwamba watu wote wanapaswa kutunza, kuelimisha na kuwaelekeza watoto katika malezi mazuri kimwili, kiroho, kiafya, kijamii na kielimu ili waweze kukuwa katika msingi mzuri utakaowafanya waweze kuendeleza au kuboresha maisha ya hapo baadae kwa kuwa watoto wa leo ndio watu wazima wa kesho.

Kujenga msingi mzuri kwa watoto kutadumisha na kuboresha maisha ya baadae.

Hivyo basi, unaalikwa kulea watoto katika maongozi mazuri ili waweze kuwa watu bora hapo baadae na waweze kuwa msaada kwa kizazi cha sasa na kizazi cha baada yao.