Kampeni ya Kutetea Wajane

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea wajane kwenye mahitaji yao ya kimwili, kiroho na kijamii hasa wale wasioweza kusimama wenyewe baada ya kuondokewa wenzi wao.

Wajane wote wanahitaji msaada hasa kipindi cha mwanzo cha ujane. Kuna wanaohitaji msaada wa kiuchumi na faraja na kuna ambao wapo vizuri kiuchumi wanahitaji msaada wa kifaraja tuu.

Kampeni hii inaamini kuwa wajane wanayo haki na nafasi sawa kama watu wengine katika jamii hata katika hali yao. Vile vile wanatamani kuishi kwa amani na furaha kwa hali ya kawaida kama watu wengine wasiokuwa wajane. Wajane wanahitaji faraja na msaada hasa pale wanaposhindwa kuishi kwa matumaini kama watu wengine kwa sababu ya kutokuwa na wenza.

Kampeni hii inahamasisha watu wote kusaidia na kuwawezesha wajane kuishi maisha bora ya matumaini yanayofaa na kutamanika na binadamu yeyote wa kawaida. Msaada wako unaweza ukawa wa kiuchumi, kimawazo au maneno, kuwapa au kuwawezesha kupata mahitaji, kuwafariji na kuwatia moyo.

Kuwasaidia na kuwafariji kunaweza kuwawezesha kuwa na amani na furaha kama watu wengine.

Hivyo basi, unaalikwa kusaidia na kuwafariji wajane ili na wao waishi kwa furaha na amani kama watu wengine bila kuhisi kupungukiwa baada ya kuwapoteza wenza wao.