Kampeni ya Kudumisha Umoja Wa Imani

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Tarehe 15/05/2012 na Melkisedeck Leon Shine.

Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Umoja bila kuangalia tofauti za imani zetu za kidini.

Kama wewe unaamini kwamba wewe umeumbwa na Mungu wako, katika imani yako. Je watu wengine wasiokuwa wa Imani yako wenye kufanana na wewe kimaumbile wameumbwa na nani? Kwa hiyo kwa nini ujenge chuki juu yao na wakati wewe na wao ni sawa?

Wote ni Binadamu, kwa nini mchukiane? Sio kazi yetu kuhukumu wengine kuwabeza na kuwadadisidadisi au kuwazarau.

Kazi yetu kuu ni kuhakikisha kama inawezekana kuwafanya wenzetu wafuate njia ile tunayofuata kwa maana tunaamini ni ya kweli.

Katika Imani zote tunafundishwa kuwa tunawajibu wa kueneza Imaniyetu kwa wengine ili wao wawe sawa na sisi na sio kujengeana chuki kwa ajili ya Imani zetu.

Huwenda yule unayemjengea chuki ungemwendea kwa amani angekuelewa na angefuata Imani yako na hivyo ungekua umemsaidia na kumjenga.

Tuwe na Amani na tuelekezane taratibu, tusijenge chuki kati yetu, tushikamane na tuwe kitu kimoja huku tukisaidiana katika ulimwengu huu mmoja.

Kumbuka chuki inaanza pale tunapoanza kudadisiana, kubishana bishana, kuzarauliana na kujiona bora kuliko wengine. Tusifanye mambo kama haya. Kila mtu na aishike Imani yake mwenyewe kwa maana ni sahihi. Usichunguze na kukwaza wengine maana kwao pia ni sahihi kama unavyoona ya kwako.

Tusitengeneze wala kuruhusu mazingira ya kukwazana kwa kuepuka kufanya mambo yanayowakwaza wengine na hasa kutoa maneno yanayowakwaza wengine. Tumpe kila mmoja uhuru wake na tutakuwa na Amani na Upendo.

Kila mtu aishi anavyojisikia, anavyotaka na anavyoamini kwa njia hii tutakuwa na Amani.

Tusalimiane na tushirikishane mabo mengine ya kimaisha bila kujali Imani zetu tukijua tuu sisi tuu wanadamu tulio sawa, kwa hiyo tupendane na tuwe na umoja.