Kampeni ya Kudumisha Amani na Upendo

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Mwaka 2014 na Melkisedeck Leon Shine.

Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Upendo bila kuangalia tofauti zetu.

Kampeni hii inaamini kuwa katika upendo kuna amani.

Kampeni hii inafundisha kwamba upendo wa kweli ni wa kuwafanyia wengine vile ungependa kufanyiwa nao. Kila mtu amfanyie mwenzake vile anavyopenda afanyiwe.

Kwa njia ya upendo kuna amani na furaha. Amani na furaha huleta mafanikio na maendeleo. Chuki na magomvi ni kikwazo cha maendeleo ya mtu binafsi na ya jamii au taifa kwa ujumla. Hii ni kwa sababu chuki na magomvi mara nyingi hubomoa na sio kujenga.

Kwa sababu ya tofauti ya matakwa yetu chuki na magomvi haziepukiki katika maisha ya binadamu. Lakini sasa ni jukumu letu kutumia njia hiyo kufahamu tofauti zetu na matakwa yetu ili tuangalie ni kwa namna gani hatuumizani sisi kwa sisi na wote tunanufaika.

Hivyo basi, unaalikwa kudumisha upendo na amani kwa kuwafanyia wengine vile unavyopenda wakufanyie. Usiruhusu tofauti za matakwa yako zikufanye kuwafanyia wengine mambo usiyopenda kufanyiwa wewe mwenyewe.