Kampeni ya Usafi Binafsi

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kudumisha usafi wao binafsi kwa afya zao na kwa maendeleo yao.

Kampeni hii inaamini kuwa usafi wa mtu binafsi unamkinga na matatizo yatokanayo na uchafu kijamii na kiafya kwa mfano maradhi ambayo yanaweza kumzuia kuendelea na kazi zake za kawaida na kukua kimaendeleo kama mtu binafsi.

Kampeni hii inafundisha kwamba usafi wa mtu binafsi ni lazima ili kujikinga na maradhi yanayoweza kukwamisha uwezo wa kuweza kufanya kazi za kila siku na kushindwa kuwa na maendeleo.

Kwa njia ya kudumisha uafi binafsi, watu wanaweza kujikinga na matatizo yatokanayo na uchafu ya kijamii na kiafya.

Hivyo basi, unaalikwa kudumisha usafi binafsi kwa afya yako na kwa maendeleo yako.