Karibu AckySHINE Charity
Kuhusu AckySHINE charity
AckySHINE charity ni nini?
AckySHINE charity ni programu ya kampeni na misaada ya kiutu ya kuhamasisha amani na umoja, kulinda mazingira na kudumisha afya na maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya jamii kwa ujumla. Kampeni hizo zinatangazwa kupitia ackyshine.com.
Lengo ni nini hasa?
Lengo la misaada na kampeni hzi ni kudumisha utu na mshikamano katika jamii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho, kwa kutunza mazingira ya asili, kulinda amani, kuhamasisha maendeleo na kudumisha afya ya mtu mmoja mmoja na ya jamii kwa ujumla.
Imeanzishwa na nani?
AckySHINE Charity ilianzishwa na inasimamiwa na Melkisedeck Leon Shine tangu 2011 hadi leo.
Melkisedeck Leon Shine
Malengo ya AckySHINE Charity
1. Kuhamasisha jamii Kudumisha Amani, upendo, umoja na Uelewano
Kufanikisha lengo hili kampeni hizi zinaendelea
2. Kuhamasisha jamii kutunza mazingira na kutumia mali asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo
Kampeni zifuatazo zinaendeshwa
1. Wanyama pori
Jinsi AckySHINE Charity inavyofanya Kazi
AckySHINE charity inatoa misaada na kufanya kampeni zake online kupitia website ya ackyshine.com. Ndani ya website hiyo matangazo ya kampeni za AckySHINE Charity yanatangazwa ili kusomwa na watembeleaji wa tovuti hiyo na hatimaye ujumbe kuwafikia.
AckySHINE Charity haifungamani wala hailengi itikadi, nchi au jamii fulani. Misaada na kampeni ni kwa watu wote kutoka nchi yoyote, kutoka jamii yoyote wenye itikadi yoyote.
AckySHINE Charity haipo kwa ajili ya kujipatia faida yoyote kifedha na haichangishi fedha, ipo kwa ajili ya kuwawezesha wanajamii kufahamu na kutenda mambo yote kwa ushirikiano katika amani na upendo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae.
Jinsi ya Kushiriki
Unaweza kushiriki kwa namna hizi;
- Kuufanyia kazi ujumbe wa kampeni husika
- Kusambaza ujumbe wa kampeni husika kwa kuwaambia watu wengine moja kwa moja au kusambaza kwenye mitandao ya Kijamii
Mafanikio Kwa Sasa
Kwa sasa kampeni zinawafikia watu zaidi ya 6000 kila mwezi.
AckySHINE Charity inalenga kuwafikia watu zaidi ya 15000 kila mwezi ifikapo mwaka 2023